137
1 Kando ya mito ya Babeli tuliketi na tulilia tulipokumbuka kuhusu Sayuni.
2 Tulitundika vinubi vyetu kwenye miti ya Babylon.
3 Huko watekaji wetu walitaka tuwaimbie, na wale walio tudhihaki walitutaka sisi tufurahi, wakisema, “Tuimbieni moja ya nyimbo za Sayuni.”
4 Tungewezaje kuimba wimbo unaomuhusu Yahwe katika nchi ya ugeni?
5 Kama nikikusahau wewe, Yerusalemu, basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake.
6 Ulimi wangu na ushikamane juu ya kinywa changu kama nisipokufikiria tena, na kama sipendelei zaidi Yerusalemu kuliko furaha yangu kuu.
7 Kumbuka, Ee Yahwe, kile walichofanya Waedomu siku ya anguko la Yerusalemu. Walisema, “Ibomoeni, ibomoeni mpaka chini kwenye misingi yake.”
8 Binti za Babeli, hivi karibuni wataharibiwa- mtu na abalikiwe, yeyote atakaye walipizia yale mliotufanyia sisi.
9 Mtu na abarikiwe, yeyote achukuaye na kusambaratisha watoto wenu juu ya jiwe.