2
1 Kwa nini mataifa wanafanya dhoruba, kwa nini watu wanafanya njama ambazo zitafeli?
2 Wafalme wa nchi kwa pamoja hushikilia misimamo yao na watawala kwa pamoja hufanya njama kinyume na Yahwe na kinyume na Masihi, wakisema,
3 “Ngoja tuzikate pingu walizo tufingia sisi na kuzitupa pingu zao.”
4 Yeye aketie katika mbingu atacheka kwa dharau mbele yao; Bwana atawadhihaki wao.
5 Kisha ataongea nao katika hasira yake na kuwaogofya kwa gadhabu yake, akisema,
6 “Mimi mwenyewe nilimpaka mafuta mfalme wa Sayuni, mlima wangu mtakatifu.”
7 Nami nitatangaza amri ya Yahwe. Yeye aliniambia, “wewe ni mwanangu! Leo hii nimekuwa baba yako.
8 Uniombe, nami nitakupa wewe taifa kwa ajili ya urithi na mikoa ya nchi iliyo bora kwa ajili ya umiliki wako.
9 Wewe utawavunja wao kwa fimbo ya chuma; kama vile mtungi wa mfinyanzi, wewe utawavunja wao vipande vipande.”
10 Hivyo sasa, ninyi wafalme; mchukue tahadhari; mjirekebishe.
11 Mwabuduni Yahwe kwa hofu na mfurahi mkitetemeka.
12 Mumbusu mwana vinginevyo atawakasirikia, na mtakufa pale pale hasira yake ikiwaka. Ni jinsi gani wamebarikiwa wale wote watafutao usalama ndani yake.