33
1 Furahini katika Yahwe, ninyi wenye haki; kusifu kwa wenye haki kwa faa sana.
2 Mshukuruni Bwana kwa kinubi; mwimbieni sifa kwa kinubi chenye nyuzi kumi.
3 Mwimbieni yeye wimbo mpaya; pigeni kwa ustadi na muimbe kwa furaha.
4 Kwa kuwa maneno ya Mungu ni ya hakika, na kila afanyacho ni haki.
5 Yeye hupenda haki na kutenda kwa haki. Dunia imejaa uaminifu wa agano la Yahwe.
6 Kwa neno la Yahwe mbingu ziliumbwa, na nyota zote ziliumbwa kwa pumzi ya mdomo wake.
7 Yeye huyakusanya maji ya baharini kama rundo; naye huiweka bahari katika ghala.
8 Basi ulimwengu wote umwogope Yahwe; wenyeji wote wa ulimwengu wamuhofu yeye.
9 Kwa maana yeye alisema, na ikafanyika; aliamuru, na ikasimama mahali pake.
10 Yahwe huvunja muungano wa mataifa; naye huishinda mipango ya wanadamu.
11 Mipango ya Yahwe husimama milele, mipango ya moyo wake ni kwa ajili ya vizazi vyote.
12 Limebarikiwa taifa ambalo Mungu wao ni Yahwe, watu ambao yeye amewachagua kama warithi wake.
13 Yahwe anatazama kutoka mbinguni; yeye huona watu wote.
14 Kutokea mahali ambapo yeye anaishi, huwatazama wote waishio juu ya nchi.
15 Yeye anaye iumba mioyo yao na kuyaona matendo yao yote.
16 Hakuna mfalme anayeokolewa na jeshi kubwa; shujaa haokolewi na nguvu zake nyingi.
17 Farasi sio salama kwa ajili ya ushindi; ijapokuwa nguvu zake ni nyingi, hawezi kuokoa.
18 Tazama, macho ya Yahwe yako kwa wale wanao mhofu yeye, wale wanao litumainia agano lake takatifu
19 kuwaokoa maisha yao na mauti na kuwaweka hai wakati wa jaa.
20 Sisi tunamngoja Yahwe, yeye ni msaada wetu na ngao yetu.
21 Mioyo yetu hufurahia ndani yake, kwa kuwa tunaamini katika jina lake takatifu.
22 Yahwe, agano lako takatifu, liwe pamoja nasi tuwekapo tumaini letu katika wewe.