34
Zaburi ya Daudi; wakati alipojifanya kuwa mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimtoa yeye nje.
1 Nitamsifu Yahwe wakati wote, siku zote sifa zake zitakuwa mdomoni mwangu.
2 Nitamsifu Yahwe! walio onewa wasikie na kufurahi.
3 Msifuni Yahwe pamoja nami, kwa pamoja tuliinue jina lake.
4 Nilimuomba Yahwe msaada naye akanijibu, akanipa ushindi juu ya hofu yangu yote.
5 Wale wanao mtazama yeye wana furaha, na nyuso zao hazina aibu.
6 Huyu mtu aliye onewa alilia na Yahwe akamsikia na kumuokoa kwenye matatizo yake yote.
7 Malaika wa Yahwe huweka kambi wakiwazunguka wale wanao muogopa yeye na kuwaokoa.
8 Onjeni muone Yahwe ni mzuri. Amebarikiwa mtu yule ambaye Yahwe ni kimbilio lake.
9 Muogopeni Yahwe, ninyi watu watakatifu wake. Hakuna kupungukikwa kwa wale wanao mhofu yeye.
10 Simba wadogo wakati mwingine hukosa chakula na kuteseka kwa njaa, bali wale wamtafutao Yahwe hawatapungukiwa chochote kilicho kizuri.
11 Njoni, wana, mnisikilize mimi. nitawafundisha ninyi hofu ya Yahwe.
12 Mtu nani aliyepo ambaye anatamani maisha na anapenda kuwa na siku nyingi, ili kwamba aweze kuona vizuri?
13 Hivyo uepushe ulimi wako na uovu na uilinde midomo yako kuongea uongo.
14 Uache uovu na utende mema. Uitafute amani na kuiendea amani.
15 Macho ya Yahwe yako kwenye haki na masikio yake huelekea kulia kwao.
16 Uso wa Yahwe uko kinyume na wale watendao uovu, kuikatilia mbali kumbukumbu yao duniani.
17 Wenye haki hulia na Yahwe husikia na kuwaokoa kwenye matatizo yao yote.
18 Yahwe yu karibu nao waliovunjika moyo, naye huwaokoa waliogandamizwa rohoni.
19 Mateso ya wenye haki ni mengi, bali Yahwe huwaokoa nayo yote.
20 Yeye huitunza mifupa yake yote, hakuna hata mmoja wao utavunjika.
21 Uovu utawauwa waovu. Wale wachukiao haki watahukumiwa.
22 Yahwe huokoa maisha ya watumishi wake. Hakuna atakaye hukumiwa hata mmoja atafutaye usalama katika yeye.