50
Zaburi ya Asafu.
1 Mungu, Mwenye nguvu, Yahwe, amenena naye aliita nchi toka mawio ya jua mpaka machweo yake.
2 Tokea Sayuni, Mungu ameangaza, ukamilifu wa uzuri.
3 Mungu wetu huja naye hakai kimya; mbele yake moto hula, na kuna dhoruba kubwa karibu naye.
4 Yeye huziita mbingu zilizo juu na nchi ili kwamba aweze kuwahukumu watu wake:
5 Kwa pamoja kusanyikeni waaminifu wangu kwangu, wale waliofanya nami agano kwa sadaka.”
6 Mbingu zitatangaza haki yake, kwa maana Mungu mwenyewe ndiye jaji. Serah
7 Sikilizeni, watu wangu, nami nitazungumza; mimi ni Mungu, Mungu wenu.
8 Sitawakaripia ninyi kwa ajili ya sadaka zenu; sadaka zenu za kuteketeza ziko nami siku zote.
9 Sitachukua ng'ombe katika nyumba yenu, wala beberu katika mazizi yenu.
10 Kwa maana kila mnyama wa msituni ni wangu, nao ng'ombe kwenye milima elfu ni wangu.
11 Ninawajua ndege wa mlimani, na wanyama pori katika shamba ni wangu.
12 Kama ningekuwa na njaa, nisingewaambia ninyi; maana ulimwengu ni wangu, na vyote vilivyomo.
13 Je! sitakula nyama ya ngombe na kunywa damu ya mbuzi?
14 Mtoleeni Mungu sadaka za shukurani, na mlipe viapo vyenu kwa Aliye Juu.
15 Mniite katika siku ya shida; nami nitawaokoa
16 Lakini kwa waovu Mungu anasema, “Inawahusu nini kuitangaza hali yangu, kwamba ninyi mmeliweka agano langu mdomoni mwenu,
17 wakati ninyi mnayachukia maelekezo na mnayatupa maneno yangu?
18 Mumuanapo mwizi, ninyi hukubaliana naye; ninyi na mnashirikiana na wale wafanyao uasherati.
19 Mwautoa mdomo wenu kwa mabaya, huelezea udanganyifu.
20 Mnakaa na kuongea dhidi ya ndugu yenu; na kukashfu mwana wa mama yenu.
21 Mmefanya mambo haya, lakini nimekaa kimya, hivyo mlidhani kuwa ni mtu flani nilliye kama ninyi mlivyo. Lakini nitawakaripia ninyi na kuwafunua, mbele ya macho yenu, mambo yote miliyofanya.
22 Mlitilie maanani hili, ninyi mnao msahau Mungu, vinginevyo nitawakata ninyi vipande vipande, na hatakuwepo yeyote wakuja kuwasaidia!
23 Yule atoaye sadaka ya shukurani hunitukuza, na yeyote apangaye njia zake katika namna iliyo sahihi nitamuonesha wokovu wa Mungu.”