51
Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi; wakati nabii Nathani amekuja kwake baada ya kusikia kuwa alilala na Bathsheba.
1 Unirehemu, Mungu, kwa sababu ya uaminifu wa agano lako; kwa ajili ya wingi wa matendo yako ya rehema, uyafute makosa yangu.
2 Unioshe kabisa uovu wangu na unisafishe dhambi zangu.
3 Kwa maana ninayajua makosa yangu, na dhambi yangu iko mbele yako siku zote.
4 Dhidi yako, wewe pekee, nimetenda dhambi na kufanya uovu mbele ya macho yako; uko sawa usemapo; wewe uko sahahi utoapo hukumu.
5 Tazama, nilizaliwa katika uovu; pindi tu mama yangu aliponibeba mimba, nilikuwa katika dhambi. Tazama, wewe unahitaji uaminifu ndani ya moyo wangu;
6 katika moyo wangu wewe utanifanya niijue hekima.
7 Unisafishe kwa hisopo, nami nitakuwa safi; unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.
8 Unifanye kusikia furaha na shangwe ili kwamba mifupa ulioivunja ifurahi.
9 Uufiche uso wako mbali na dhambi zangu na uyafute maovu yangu yote.
10 Uniumbie moyo safi, Mungu, na uifanye upya roho ya haki ndani yangu.
11 Usiniondoe uweponi mwako, na usimuondoe roho Mtakatifu ndani yangu.
12 Unirudishie furaha ya wokovu wako, na unihifadhi mimi kwa roho ya utayari.
13 Ndipo nitawafundisha wakosaji jia zako, na wenye dhambi watakugeukia wewe.
14 Unisamehe kwa ajili ya umwagaji damu, Mungu wa wokovu wangu, nami nitapiga kelele za shangwe ya haki yako.
15 Ee Bwana, uifungue midomo yangu, na mdomo wangu itazieleza sifa zako.
16 Kwa maana wewe haufurahishwi katika sadaka, vinginevyo ningekutolea sadaka; wewe hauwi radhi katika sadaka ya kuteketezwa.
17 Sadaka ya Mungu ni roho iliyovunjika. Wewe, Mungu hautadharau moyo uliopondeka na kujutia.
18 Uitendee mema Sayuni katika nia yako nzuri; uzijenge tena kuta za Yerusalem.
19 Kisha wewe utafurahia sadaka yenye haki, katika sadaka za kuteketeza; ndipo watu wetu watatoa ng'ombe kwenye madhabahu yako.