60
Kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye Shushan Eduth. Zaburi ya Daudi, kwa ajili ya kufundisha. Wakati alipopigana na Aram Naharaim pamoja na Aram Zobah, na Joab walirudi na kuwaua Wendomi elfu kumi na mbili katika bonde la chumvi.
1 Mungu, wewe umetutupa; umeuvunja ulinzi wetu; wewe umekuwa hasirani; utuwezeshe tena.
2 Wewe umeifanya nchi kutetemeka; umeipasua pasua; uiponye nyufa zake, maana zinatikisika.
3 Wewe umewafanya watu wako kuona mambo magumu; umetufanya tunywe mvinyo wenye kutufanya kupepesuka.
4 Kwa wale wanao kuheshimu wewe, wewe umeweka bandera ionekane dhidi ya wale wabebao upinde. Selah
5 Ili kwamba wale uwapendao waweze kuokolewa, utuokoe sisi kwa mkono wako wa kuume na unijibu.
6 Mungu ameongea katika utakatifu wake, “Nitashangilia; nitaigawanya Shekemu na kuligawa bonde la Sukothi.
7 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu na Ephraimu pia ni kofia yangu ya chuma; Yuda ni fimbo yangu ya kifalme.
8 Moabu ni bakuli langu la kunawia; juu ya Edomu nitatupa kiatu changu; nitapiga kelele za ushindi kwa sababu ya Filisti.”
9 Ni nani atakaye nileta kwenye mji imara? Ni nani ataniongoza kwenda Edomu?
10 Lakini wewe, Mungu, je, haukutukataa? Wewe hauendi vitani pamoja na jeshi letu.
11 Utusaidie dhidi ya adui yetu, maana msaada wa mwanadamu ni bure.
12 Kwa msaada wa Mungu tutashinda; yeye atawakanyaga chini adui zetu.