61
Kwa kiongozi wa muziki; kwenye chombo cha nyuzi. Zaburi ya Daudi.
1 Sikia kulia kwangu, shughulikia maombi yangu.
2 Kutokea mwisho wa nchi nitakuita wewe wakati moyo wangu umeelemewa; uniongoze kwenye mwamba ulio juu kuliko mimi.
3 Maana wewe umekuwa kimbilio langu la usalama, nguzo imara dhidi ya adui.
4 Uniache niishi hemani mwako milele! Nipate kimbilio salama chini ya makazi ya mbawa zako. Selah
5 Kwa kuwa wewe, Mungu, umesikia viapo vyangu, wewe umenipa mimi urithi wa wale wanao liheshimu jina lako.
6 Wewe utaongeza maisha ya mfalme; miaka yake itakuwa kama vizazi vingi.
7 Yeye atabakia mbele ya Mungu milele.
8 Nitaliimbia sifa jina lako milele ili kwamba niweze kufanya viapo vyangu kila siku.