80
Kwa kiongozi wa muziki, seti kwenye mtindo wa Shoshannim Eduth. Zaburi ya Asafu.
1 Usikie, Mchungaji wa Israel, wewe uliye muongoza Yusufu kama kundi; wewe uketiye juu ya makerubi, utuangazie!
2 Machoni pa Efraimu na Benjamini na Manase, uziinue nguvu zako; njoo na utuokoe.
3 Mungu, uturejeshe sisi; uangaze uso wako juu yetu, nasi tutaokolewa.
4 Yahwe Mungu wa majeshi, mpaka lini utawakasirikia watu wako wanapoomba?
5 Umewalisha wa mkate wa machozi na umewapa machozi ili wanywe katika kiasi kikubwa.
6 Umetufanya kitu kwa ajili ya majirani zetu kubishania, na maadui zetu hucheka kuhusu sisi kati yao.
7 Mungu wa majeshi, uturejeshe sisi; nasi tutaokolewa.
8 Wewe ulileta mzabibu kutoka Misri; ukawafukuza mataifa na ukaupanda.
9 Uliisafisha ardhi kwa ajil yake; nao ulipata mzizi na kuijaza nchi.
10 Milima ilifunikwa kwa kivuli chake, mierezi ya Mungu kwa matawi yake.
11 Ilieneza matawi yake mbali kama bahari na mashina yake mpaka kwenye Mto Euphrates.
12 Kwa nini umezibomoa kuta zake hata wapitao karibu huyachuma matunda yake.
13 Ngurue wa msituni wanauharibu, na wanyama wa kondeni wanaula.
14 Urudi, Ee Mungu wa majeshi; kutoka mbinguni utazame chini na uuangalie na kuujali huu mzabibu.
15 Huu ni mzizi ambao mkono wako wa kuume umeupanda, mashina ambayo wewe uliyafanya yakue.
16 Yamekatwa na kuchomwa; yameangamia kwa sababu ya kukemea kwako.
17 Mkono wako na uwe juu ya mtu aliye mkono wako wa kuume, kwa mwana wa mtu uliyemfanya imara kwa ajili yako mwenyewe.
18 Ndipo hatuta kuacha wewe; utuhuishe, nasi tutaliita jina lako.
19 Yahwe, Mungu wa majeshi, uturejeshe sisi; utuangazie nuru ya uso wako, nasi tutaokolewa.