81
Kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye mtindo wa Gittith.
1 Mwimbieni Mungu aliye nguvu yetu kwa sauti; pigeni kelele za furaha kwa Mungu wa Yakobo.
2 Imbeni wimbo na pigeni matari, kinubi chenye sauti nzuri pamoja na kinanda.
3 Pigeni panda mwandamo wa mwezi, katika siku ya mbalamwezi, mwanzoni mwa sikukuu.
4 Kwa kuwa ni agizo kwa Israeli, amri iliyotolewa na Mungu wa Yakobo.
5 Aliitoa kama maelekezo kwa Yusufu alipoenda katika nchi ya Misri, ambako nilisikia sauti ambayo sikuweza kuitambua:
6 “Niliutua mzigo kutoka mabegani mwake; mikono yake ilipumzishwa kubeba kikapu.
7 Katika dhiki yako uliniita, nami nikakusaidia; nilikujibu kutoka katika wingu jeusi la radi. Nilikujaribu kwenye maji ya Meriba. Selah
8 Sikilizeni, watu wangu, nami nitawaonya, Israeli, kama tu ugalinisikiliza!
9 Lazima kati yenu kusiwepo na mungu wa kigeni; haupaswi kumwabudu mungu wa kigeni.
10 Mimi ni Yahwe niliyekutoa katika nchi ya Misri, fungua sana kinywa chako, nami nitakijaza.
11 Lakini watu wangu hawakusikiliza maneno yangu; Israeli hawakunitii.
12 Nikawaacha waende katika katika njia yao wenyewe ya ukaidi ili kwamba waweze kufanya kinachoonekana sahihi kwao.
13 Oh, laiti watu wangu wangenisikiliza mimi; oh, watu wangu wangelitembea katika njia yangu.
14 Kisha ningewatiisha adui zao haraka na kugeuzia mkono wangu dhidi ya watesi wao.
15 Wale wanaomchukia Yahwe katika hofu na waanguke chini mbele zake! Wawe wanyonge milele.
16 Ningewalisha Israeli kwa ngano bora; Ningewatosheleza kwa asali itokayo mwambani.”