82
Zaburi ya Asafu.
1 Mungu amesimama katika kusanyiko la mbinguni; katikati ya miungu anahukumu.
2 Hata lini mtahukumu bila haki na kuonesha upendeleo kwa waovu? Selah
3 Wateteeni maskini na yatima; dumisheni haki kwa aliyetaabishwa na fukara.
4 Muokoeni maskini na muhitaji; watoeni mkononi mwa waovu.
5 Hawajui wala hawaelewi; hutembea gizani; misingi yote ya nchi imebomoka.
6 Mimi nilisema, “Ninyi ni miungu, na ninyi nyote wana wa Mungu aliye Juu.
7 Hata hivyo mtakufa kama wanadamu na mtaanguka kama mmoja wa wakuu.”
8 Uinuke, Ee Mungu, uihukumu nchi, maana unaurithi katika mataifa yote.