83
Wimbo. Zaburi ya Asafu.
1 Ee Mungu, usikae kimya! usitupuuze na kustarehe, Ee Mungu.
2 Tazama, adui zako wanafanya vurugu, na wale wakuchukiao wameinua vichwa vyao.
3 Wanafanya hila juu ya watu wako na kwa pamoja kupanga njama dhidi ya wale uwalindao. Wamesema,
4 “Njoni na tuwaangamize wao kama taifa. Kisha jina la Israeli halitakumbukwa.”
5 Wamepanga njama pamoja wakiwa na mkakati mmoja; wamefanya muungano dhidi yako.
6 Hii inajumuisha hema za Edomu na Waishmaeli, na watu wa Moabu na Wahagari, ambao wamepanga njama pamoja nao
7 Gebal, Amoni, Amaleki; pia inajumuisha Filisti na wenyeji wa Tiro.
8 Ashuri pia ameshirikina nao; wanawasaidia wana wa Lutu. Serah
9 Ufanye kwao kama ulivyofanya kwa Midiani, kama ulivyofanya kwa Sisera na kwa Yabini kwenye Mto Kishoni.
10 Waliangamizwa kule Endori na wakawa kama mbolea juu ya chi.
11 Uvifanye vyeo vyao kama Oreb na Zeeb, na wakuu wao wote kama Zeba na Zalmuna.
12 Wao walisema, natujimilikishe malisho ya Mungu.”
13 Ee Mungu wangu, uwafanye kama mavumbi ya kisulisuli, kama makapi mbele ya upepo,
14 Kama moto uteketezao msitu, na kama miali ya moto iwakayo milimani.
15 Uwafuatie kwa tufani yako, na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.
16 Uwajaze nyuso zao kwa aibu ili kwamba waweze kulitafuta jina lako, Yahwe.
17 Nao waaibishwe na kufadhaishwa milele; waangamizwe katika aibu.
18 Kisha watajua kwamba ni wewe pekee, Yahwe, Uliye Juu ya nchi yote.