84
Kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye mtindo wa Gittith. Zaburi ya wana wa Kora.
1 Ni jinsi gani maskani yako yapendeza, Ewe Yahwe wa Majeshi!
2 Ninashauku ya kuingia nyumbani mwa Yahwe, nimechoka sana kwa sababu ninatamani sana kuwa nyumani mwako. Moyo wangu na mwili wangu wote wakuita wewe Mungu uliye hai.
3 Hata Shomoro naye amepata nyumba yake na mbayuwayu amejipatia kiota kwa ajili yake mwenyewe mahali awezapo aweza kuweka makinda yake karibu na madhabahu yako, Ee Yahwe wa majeshi, Mfalme wangu, na Mungu wangu.
4 Wamebarikiwa wale ambao huishi katika nyumba yako; nao hukusifu wewe siku zote. Selah
5 Amebarikiwa mtu yule ambaye nguvu zake ziko katika wewe, katika moyo wake mna njia kuu ziendazo mpaka Sayuni.
6 Wanapopita katika bonde la machozi, hupata chemchem ya maji kwa ajili ya kunywa. Mvua ya vuli hulivika baraka.
7 Huendelea toka nguvu hadi nguvu; kila mmoja wao katika sayuni huonekana mbele ya Mungu.
8 Yahwe Mungu wa majeshi, sikia maombi yangu; Mungu wa Yakobo, usikilize nisemacho! Selah
9 Ee Mungu, uiangalie ngao yetu; uwaangalie wapakwa mafuta wako.
10 Kwa maana siku moja katika nyumba yako ni bora kuliko siku elfu mahali pengine. Ni bora niwe mlinzi wa mlango katika nyumba ya Mungu wangu, kuliko kuishi katika mahema ya waovu.
11 Kwa kuwa Yahwe Mungu ni jua letu na ngao yetu; Yahwe atatoa neema na utukufu; hazuii zuri lolote kwa wale ambao hutembea katika uadilifu.
12 Yahwe wa majeshi, amebarikiwa mtu yule anaye kutumainia wewe.