85
Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya wana wa Kora.
1 Yahwe, wewe umeonesha fadhilia kwenye nchi yako; umeurejesha ustawi wa Yakobo.
2 Umesamehe dhambi ya watu wako; umezisitiri dhambi zao zote. Selah
3 Umeondoa ghadhabu yako yote; umeiacha hasira yako kali.
4 Uturejeshe sisi, Ee Mungu wa wokovu wetu, na uikomeshe chuki yako juu yetu.
5 Je! Utaendelea kuwa na hasira juu yetu milele? utadumisha hasira kizazi chote kijacho?
6 Je, hautatuhuisha tena? Kisha watu wako watafurahia katika wewe.
7 Utuoneshe sisi uaminifu wa agano lako, Yahwe, utupe sisi wokovu wako.
8 Nitasikiliza yale Yahwe Mungu asemayo, maana yeye atafanya amani pamoja na watu wake, wafuasi wake waminifu. Lakini lazima wasirudi tena katika njia za kipumbavu.
9 Hakika wokovu wake u karibu na wale wanao mwabudu yeye; kisha utukufu utabaki katika nchi yetu.
10 Uaminifu wa agano na uaminifu vimekutana pamoja; haki na amani vimebusiana.
11 Uaminifu unatoa chemchem kutoka ardhini, na haki hutazama chini kutoka mawinguni.
12 Ndiyo, Yahwe atatoa baraka zake njema, na nchi itatoa mazao yake.
13 Haki itaenda mbele zake na kufanya njia kwa ajili ya nyayo zake.