9
Kwa kiongozi wa muziki; weka kwenye mtindo wa Muth Labben. Zaburi ya Daudi.
1 Nitamshukuru Yahweh kwa moyo wangu wote; nitayasimulia matendo yako makuu.
2 Nitafurahi na kushangilia katika wewe; nitaliimbia jina lako, Wewe uliye juu.
3 Maadui zangu wanaponirudia, hujikwaa na kuangamia mbele zako.
4 Kwa kuwa umenitetea kwa haki; unakaa kwenye kiti chako cha enzi, ukihukumu kwa haki!
5 Uliwakemea mataifa; umewaharibu waovu; na kuwa futilia mbali jina lao milele na milele.
6 Maadui wamebomoka kama magofu ulipo pindua miji yao. Kumbukumbu yao yote imepotea.
7 Bali Yahweh anadumu milele; ameweka kiti chake cha enzi kwa ajili ya haki.
8 Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki, na atatekeleza hukumu kwa ajili ya mataifa kwa haki.
9 Yahweh pia atakuwa ngome kwake aliye onewa, na ngome wakati wa shida.
10 Wale wakujuao jina lako wanaamini katika Wewe, kwa ajili yako, Yahweh, usiwaache wale wakutafutao.
11 Mwibieni sifa Yahweh, anaye tawala katika Sayuni; waambieni mataifa yale aliyo yatenda.
12 Kwa kuwa Mungu alipizae kisasi cha damu hukumbuka; naye hasahau kilio cha anayeonewa.
13 Unihurumie, Yahweh; tazama vile ninavyo onewa na wale wanao nichukia, wewe ambaye unaweza kunikwapua katika lango la kifo.
14 Oh, ili niweze kutangaza sifa zako. Katika lango la binti sayuni nitaufurahia wokovu wako!
15 Mataifa yamedidimia chini katika shimo ambalo walilolitengeneza; miguu yao imenaswa kwenye nyavu walioificha wenyewe.
16 Yahweh amejidhihilisha; na kutekeleza hukumu; waovu wameangamia kwa matendo yao wenyewe. Selah
17 Waovu wamekataliwa na kupelekwa kuzimu, mataifa yote yanayo msahau Mungu.
18 Kwa kuwa mhitaji hata sahauliwa siku zote, wala matumaini ya wanyonge hayatapotea milele.
19 Inuka, Yahweh, usimruhusu mtu kutushinda; mataifa na wahukumiwe mbele zako.
20 Bwana, waogopeshe; mataifa waweze kutambua kuwa ni wanadamu tu. Selah