23
1 Haya ni maneno ya mwisho ya Daudi-Daudi mwana wa Yese, mtu aliyeheshimiwa sana, aliyetiwa mafuta na Mungu wa Yakobo, mwandishi mzuri wa zaburi wa Israeli.
2 “Roho ya Yahwe alisema nami, na neno lake lilikuwa ulimini mwangu.
3 Mungu wa Israeli alinena, Mwamba wa Israeli aliniambia, “Atawalaye kwa haki juu yangu, atawalaye katika hofu ya Mungu.
4 Atakuwa kama nuru ya asubuhi jua linapochomoza, asubuhi isiyo na mawingu, wakati mche mwororo unapochipua kutoka ardhini kupitia mwangaza wa mng'ao wa jua baada ya mvua.
5 Hakika, je familia yangu haiko hivi mbele za Mungu? Je hajafanya nami agano la milele, taratibu la uhakika kwa kila njia? Je yeye haongezi wokovu wangu na kutimiza kila hitaji langu?
6 Lakini yasiyofaa yote yatakuwa kama miiba na kutupwa mbali, kwa maana haiwezekani kukusanywa kwa mikono.
7 Ayagusaye ni lazima atumie chombo cha chuma au au fumo la mkuki. Ni lazima yachomwe mahali yalipo.
8 Haya ni majina ya askari wa Daudi: Yashobeamu Mhakmoni alikuwa kiongozi wa mashujaa. Aliua watu mia nne wakati mmoja.
9 Baada yake alikuwa Elieza mwana wa Dodo, mwana wa mwahohi, mmoja wa mashujaa watatu wa Daudi. Alikuwepo walipowashinda Wafilisti waliokuwa wamekusanyika kwa vita, na wakati watu wa Israeli walipokuwa wamekimbia.
10 Elieza akasimama na kuwapiga Wafilisti mpaka mkono wake ukachoka, mpaka mkono wake ukang'ang'ania mpini wa upanga wake. Siku hiyo Yahwe akatoa ushindi mkuu. Jeshi likarejea kwa ajili ya kuteka tu nyara za waliouawa na Elieza.
11 Baada yake alikuwa Shama mwana wa Agee, Mharari. Wafilisti wakajikusanya pamoja palipokuwa na shamba la dengu, na jeshi likawakimbia.
12 Lakini Shama akasimama katikati ya shamba na kulitetea. Aliwauwa Wafilisti, na Yahwe akaleta ushindi mkuu.
13 Watatu kati ya askari thelathini walishuka kwa Daudi nyakati za mavuno, katika pango la Adulamu. Jeshi la Wafilisti lilikuwa limepiga kambi katika bonde la Mrefai.
14 Wakati huo Daudi alikuwa katika ngome yake, pangoni, wakati Wafilisti walikuwa wanaimilk Bethlehemu.
15 Daudi alitamani maji na akasema, “Kama ingekuwa mtu mmoja angenipa maji ya kunywa kutoka kisima kilichopo Bethlehemu, kisima kilichopo langoni!”
16 Hivyo mashujaa hawa watatu wakapita kati ya jeshi la Wafilisti na kuchota maji katika kisima cha Bethlehemu, kilichopo langoni. Wakachukua maji na kuyaleta kwa Daudi, lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake akayamwaga mbele za Yahwe.
17 Kisha akasema, “Iwe mbali nami, Yahwe, kwamba niyanywe haya. Je ninywe damu ya watu waliohatarisha maisha yao?” Hivyo akakataa kuyanywa. Haya ni mambo yaliyofanywa na mashujaa watatu.
18 Abishai, nduguye Yoabu na mwana wa Seruya, alikuwa akida wa watatu. Alipigana kwa mkuki wake na watu mia tatu na akawauwa wote mara. Mara kwa mara alitajwa kati ya mashujaa watatu.
19 Hakuwa maarufu kuliko wale watatu? Alifanywa akida wao. Lakini, umaarufu wake haukulingana na umaarufu wa wale mashujaa watatu.
20 Benaya kutoka Kabseeli mwana wa Yehoyada; alikuwa mtu hodari aliyefanya matendo makuu. Aliwauwa wana wawili wa Arieli wa Moabu. Pia alishuka shimoni na kuuwa simba wakati wa theruji.
21 Na alimwua Mmisri aliyekuwa mtu mnene sana. Mmisri alikuwa na mkuki mkononi, lakini Benaya alipigana naye kwa fimbo tu. Aliuchukua mkuki mkononi mwa Mmisri na kisha kumwua nao.
22 Benaya mwana wa Yehoyada alifanya matendo haya, naye alitajwa kati ya mashujaa watatu.
23 Alikuwa na heshima kuliko mashujaa thelathini kwa ujumla wao, lakini hakuwa na heshima kama wale mashujaa watatu. Hata hivyo Daudi alimweka kuwa mlinzi wake.
24 Wafuatao ni wale watu thelathini: Asaheli nduguye Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu,
25 Shama Mharodi, Elika Mharodi,
26 Helesi Mpeloni, Ira mwana wa Ikeshi Mtekoi,
27 Abi Ezeri Mwanathothi, Mebunai Mhushathi,
28 Salmoni Mhahoi, Maharai Mnetofathi;
29 Helebu mwana wa Baana, Mnetofathi, Itai mwana wa Rabai kutoka Gibea ya Wabenjamini,
30 Benaya Mpirathoni, Hidai wa mabonde ya Gaashi.
31 Abieliboni Mwarbathi, Azmawethi Mbarhumi,
32 Eliaba Mshalboni, wana wa Yasheni, Yonathani mwana wa Shama Mharari;
33 Ahiamu mwana wa Sharari Mharari,
34 Elifeleti mwana wa Ahasbai Mmaakathi, Eliamu mwana wa Ahithofeli Mgiloni,
35 Hezro Mkarmeli, Parai Mwarbi,
36 Igali mwana wa Nathani kutoka Soba, Bani kutoka kabila la Gadi,
37 Zeleki Mwamoni, Naharai Mbeerothi, mbeba silaha wa Yoabu mwana wa Seruya,
38 Ira Mwithri, Garebu Mwithri,
39 Uria Mhiti - jumla yao thelathini na wanane.