5
1 Kisha nikageuka na kuinua macho yangu, nami nikaona, tazama, gombo lirukalo!
2 Malaika akaniuliza, “Unaona nini?” Nikajibu, “Ninaona gombo lirukalo, urefu wake dhiraa ishirini na upana wake dhiraa kumi.”
3 Ndipo aliponiambia, “Hii ni laana iendayo juu ya uso wa nchi yote, kwani tangu sasa kila mwivi ataondolewa kulingana na lisemavyo upande mmoja, wakati kila aapaye kiapo cha uongo ataondolewa kulingana na lisemavyo upande mwingine, kwa kadili ya maneno yake.
4 “Nitalituma - asema Yahwe wa majeshi - hivyo litaingia nyumbani mwa mwivi na nyumbani mwa aapaye kwa uongo kwa jina langu. Litasalia nyumbani mwake na kuteketeza mbao na mawe yake.”
5 Ndipo malaika aliyekuwa akisema nami alipoenda nje na kuniambia, “Inua macho yako uone kinachokuja!”
6 Nikasema, “Ni nini hiki?” Akasema, “Hiki ni kikapu kilicho na efa ijayo. Huu ni uovu wao katika nchi yote.”
7 Kisha mfuniko wa risasi ukainuliwa kutoka ndani ya kikapu na kulikuwa na mwanamke chini yake amekaa ndani yake!
8 Malaika akasema, “Huu ni uovu!” na akamtupa tena kikapuni, na kurusha mfuniko wa risasi mlango pake.
9 Nilipoinua macho nikaona wanawake wawili wakija kwangu, na upepo ulikuwa ndani ya mabawa yao - walikuwa na mabawa kama mabawa ya korongo. Wakainua kikapu kati ya mbingu na nchi.
10 Hivyo nikamwuliza malaika aliyesema nami, “Wanapeleka wapi kikapu?”
11 Akaniambia, “Wanakwenda kujengea hekalu katika nchi ya Shinari kwa ajili yake, hekalu litakapokuwa tayari, kikapu kitawekwa kwenye msingi ulioandaliwa kwa ajili yake.”