6
1 Kisha nikageuka na kuinua macho na nikaona vibandawazi vinne vya farasi vikija kutoka kati ya milima miwili; na milima hiyo ilikuwa imetengenezwa kwa shaba.
2 Kibandawazi cha kwanza kilikuwa na farasi wekundu, kibandawazi cha pili kilikuwa na farasi weusi,
3 kibandawazi cha tatu kilikuwa na farasi weupe, na kibandawazi cha nne kilikuwa na farasi wa kijivu.
4 Hivyo nikamwuliza malaika aliyesema nami, “Ni vitu gani hivi bwana wangu?”
5 Malaika akajibu na kuniambia, “Hizi ni pepo nne za mbinguni zisimamazo mbele ya Bwana wa dunia yote.
6 Lenye farasi weusi linakwenda nchi ya kaskazini; farasi weupe wanakwenda nchi ya magharibi; na farasi wa kijivu wanakwenda nchi ya kusini.”
7 Farasi hawa wenye nguvu walitoka na wanatafuta kwenda na kuzunguka juu ya nchi, hivyo malaika akasema, “Nendeni na mzunguke juu ya nchi!” nao wakaenda juu ya dunia yote.
8 Kisha akaniita na kuniambia, “Tazama wale wanaokwenda nchi ya kaskazini, wataituliza roho yangu juu nchi hiyo.”
9 Hivyo neno la Yahwe likanijia kusema,
10 “Chukua sadaka kutoka kwa waliohamishwa - kutoka kwa Helidai, Tobiya na Yedaya - leo hii uende na kuipeleka katika nyumba ya Yosia mwana wa Zefania, aliyetoka Babeli.
11 Kisha uchukue fedha na dhahabu, ufanye taji na uivike katika kichwa cha Yoshua mwana wa Yehosadaki kuhani mkuu.
12 Ongea naye na useme, Yahwe wa majeshi asema hivi: Mtu huyu, jina lake Tawi! Naye atakuwa alipo na kisha atajenga hekalu la Yahwe!
13 Ndiye atakayejenga hekalu la Yahwe naye atauinua utukufu wake; kisha ataketi na kutawala katika kiti chake cha enzi. Atakuwa kuhani juu ya kiti cha enzi na ufahamu wa amani utakuwa kati ya vyote viwili.
14 Taji itawekwa hekaluni mwa Yahwe kwa heshima ya Heldai, Tobiya na Yedaya na kama kumbukumbu ya ukarimu wa mwana wa Zefania.
15 Ndipo waliombali watakapokuja na kulijenga hekalu la Yahwe, hivyo mtajua kuwa Yahwe wa majeshi amenituma kwenu; kwani ikiwa kweli mnaisikiliza sauti ya Yahwe Mungu wenu hili litatendeka!”