1 Mambo Ya Nyakati
1
Kumbukumbu Za Historia Kuanzia Adamu Hadi Abrahamu
(Mwanzo 5:1-32; 10:1-32; 11:10-26)
Adamu Hadi Wana Wa Noa
Adamu, Sethi, Enoshi, Kenani, Mahalaleli, Yaredi, Enoki, Methusela, Lameki, Noa.
 
Wana wa Noa walikuwa:
Shemu, Hamu na Yafethi.
Wana Wa Yafethi
Wana wa Yafethi walikuwa:
Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.
Wana wa Gomeri walikuwa:
Ashkenazi, Rifathi na Togarma.
Wana wa Yavani walikuwa:
Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu.
Wana Wa Hamu
Wana wa Hamu walikuwa:
Kushi, Misraimu,* Yaani Misri. Putu na Kanaani.
Wana wa Kushi walikuwa:
Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka.
Wana wa Raama walikuwa:
Sheba na Dedani.
10 Kushi akamzaa
Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa katika nchi.
11 Misraimu akawazaa:
Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, 12 Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori.
13 Wana wa Kanaani walikuwa:
Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi, 14 Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, 15 Wahivi, Waariki, Wasini, 16 Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.
Wana Wa Shemu
17 Wana wa Shemu walikuwa:
Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.
Wana wa Aramu walikuwa:
Usi, Huli, Getheri na Mesheki.
18 Arfaksadi akamzaa Shela,
Shela akamzaa Eberi.
19 Eberi alipata wana wawili:
Mmoja wao aliitwa Pelegi, Pelegi maana yake Mgawanyiko. kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.
20 Wana wa Yoktani walikuwa:
Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, 21 Hadoramu, Uzali, Dikla, 22 Obali, Abimaeli, Sheba, 23 Ofiri, Havila na Yobabu. Wote hawa walikuwa wana wa Yoktani.
 
24 Wana wa Shemu walikuwa Arfaksadi, Shela,
25 Eberi, Pelegi, Reu,
26 Serugi, Nahori, Tera,
27 Tera akamzaa Abramu (yaani, Abrahamu).
Jamaa Ya Abrahamu
28 Abrahamu alikuwa na wana wawili:
Isaki na Ishmaeli.
Wazao Wa Hagari
(Mwanzo 25:12-16)
29 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Hagari:
Nebayothi mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Kedari, Adbeeli, Mibsamu, 30 Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema, 31 Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.
Wazao Wa Ketura
32 Wana waliozaliwa na Ketura suria wa Abrahamu walikuwa:
Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua.
Wana wa Yokshani walikuwa:
Sheba na Dedani.
33 Wana wa Midiani walikuwa:
Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa.
Wote hao walikuwa wa uzao wa Ketura.
Wazao Wa Sara
34 Abrahamu alikuwa baba wa Isaki.
Wana wa Isaki walikuwa:
Esau na Israeli.
Wana Wa Esau
(Mwanzo 36:1-19)
35 Wana wa Esau walikuwa:
Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora.
36 Wana wa Elifazi walikuwa:
Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi;
Elifazi kwa Timna akamzaa Amaleki.
37 Wana wa Reueli walikuwa:
Nahathi, Zera, Shama na Miza.
Watu Wa Seiri Waliokuwa Edomu
(Mwanzo 36:20-30)
38 Wana wa Seiri walikuwa:
Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani.
39 Wana wa Lotani walikuwa wawili:
Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna.
40 Wana wa Shobali walikuwa:
Alvani, Maandishi ya Kiebrania yanamwita Alian. Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.
Wana wa Sibeoni walikuwa:
Aiya na Ana.
41 Mwana wa Ana alikuwa:
Dishoni.
Nao wana wa Dishoni walikuwa:
Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.
42 Wana wa Eseri walikuwa:
Bilhani, Zaavani na Akani.
Wana wa Dishani walikuwa:
Usi na Arani.
Watawala Wa Edomu
(Mwanzo 36:31-43)
43 Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli:
Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba.
44 Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.
45 Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.
46 Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.
47 Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.
48 Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati, akawa mfalme baada yake.
49 Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.
50 Baal-Hanani alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu. 51 Naye Hadadi pia akafa.
 
Wakuu wa Edomu walikuwa:
Timna, Alva, Yethethi, 52 Oholibama, Ela, Pinoni, 53 Kenazi, Temani, Mibsari, 54 Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu.

*1:8 Yaani Misri.

1:19 Pelegi maana yake Mgawanyiko.

1:40 Maandishi ya Kiebrania yanamwita Alian.