5
Mwasherati atengwe
Yamkini habari imeenea ya kuwa miongoni mwenu kuna uzinzi ambao haujafanyika hata miongoni mwa watu wasiomjua Mungu: Kwamba mtu anaishi na mke wa baba yake. Nanyi mwajivuna! Je, haiwapasi kuhuzunika na kumtenga na ushirika wenu mtu huyo aliyefanya mambo hayo? Hata kama siko pamoja nanyi katika mwili, niko nanyi katika roho. Nami nimekwisha kumhukumu mtu huyo aliyetenda jambo hili, kama vile ningekuwepo. Mnapokutana katika Jina la Bwana wetu Isa nami nikiwepo pamoja nanyi katika roho, na uweza wa Bwana Isa ukiwepo, mkabidhini mtu huyu kwa Shetani, ili mwili wake uharibiwe, lakini roho yake iokolewe katika siku ya Mwenyezi Mungu.
Majivuno yenu si mazuri. Je, hamjui kwamba chachu kidogo huchachusha donge zima la unga? Ondoeni chachu ya kale ili mpate kuwa donge jipya lisilotiwa chachu, kama vile mlivyo. Kwa maana Al-Masihi, Mwana-Kondoo wetu wa Pasaka*Sherehe iliyowakumbusha Waisraeli jinsi Mwenyezi Mungu alivyowakomboa kutoka utumwani huko Misri. amekwisha tolewa kuwa dhabihu. Kwa hiyo, tusiiadhimishe sikukuu hii kwa chachu ya zamani, chachu ya nia mbaya na uovu, bali kwa mkate usiotiwa chachu, ndio weupe wa moyo na kweli.
Niliwaandikia katika waraka wangu kuwa msishirikiane na wazinzi. 10 Sina maana kwamba msishirikiane na wazinzi wa ulimwengu huu, au wenye tamaa mbaya, wanyang’anyi au waabudu sanamu. Kwa kufanya hivyo ingewalazimu mtoke ulimwenguni humu. 11 Lakini sasa nawaandikia kwamba msishirikiane na mtu yeyote anayejiita ndugu, hali akiwa ni mzinzi, au mwenye tamaa mbaya, mwabudu sanamu au msingiziaji, mlevi au mdhalimu. Mtu kama huyo hata msile naye.
12 Yanihusu nini kuwahukumu wale watu walio nje ya kundi la waumini? Je, si mnapaswa kuwahukumu hao walio ndani? 13 Mungu atawahukumu hao walio nje. “Ninyi mwondoeni huyo mtu mwovu miongoni mwenu.”

*5:7 Sherehe iliyowakumbusha Waisraeli jinsi Mwenyezi Mungu alivyowakomboa kutoka utumwani huko Misri.