19
Mgawo kwa Simeoni
Kura ya pili ikaangukia kabila la Simeoni, kufuatana na koo zao. Urithi wao ulikuwa ndani ya eneo la Yuda. Ulijumuisha:
Beer-Sheba (au Sheba), Molada, Hasar-Shuali, Bala, Esemu, Eltoladi, Bethuli, Horma, Siklagi, Beth-Markabothi, Hasar-Susa, Beth-Lebaothi na Sharuheni; hii ilikuwa miji kumi na tatu pamoja na vijiji vyake.
Pia Aini, Rimoni, Etheri, na Ashani; hii ilikuwa miji minne na vijiji vyake, pamoja na vijiji vyote vinavyoizunguka miji hii hadi Baalath-Beeri (ambayo ndiyo Rama iliyo katika Negebu).
Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Simeoni kufuatana na koo zao. Urithi wa Wasimeoni ulitolewa kutoka fungu la Yuda, kwa kuwa fungu la Yuda lilikuwa kubwa kuliko walivyohitaji. Hivyo kabila la Simeoni lilipewa urithi wao ndani ya eneo la Yuda.
Mgawo kwa Zabuloni
10 Kura ya tatu ikaangukia kabila la Zabuloni, kufuatana na koo zao:
Mpaka wa urithi wao uliendelea hadi Saridi. 11 Kuelekea upande wa magharibi ukafika Marala, ukagusa Dabeshethi, na kuendelea hadi kwenye bonde karibu na Yokneamu. 12 Ukageuka mashariki, kuanzia Saridi kuelekea mawio ya jua hadi kwenye nchi ya Kisiloth-Tabori, na kwenda hadi Daberathi, kupanda Yafia. 13 Kisha ukaendelea mashariki hadi Gath-Heferi na kufika Eth-Kasini, ukatokea Rimoni na kugeuka kuelekea Nea. 14 Huko mpaka ukazungukia upande wa kaskazini hadi Hanathoni na kuishia katika Bonde la Ifta-Eli.
15 Miji mingine iliyojumuishwa ni Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala na Bethlehemu. Kulikuwa na miji kumi na mbili pamoja na vijiji vyake.
16 Miji hii na vijiji vyake ilikuwa urithi wa Zabuloni, kufuatana na koo zao.
Mgawo kwa Isakari
17 Kura ya nne ikaangukia kabila la Isakari, kufuatana na koo zao. 18 Eneo lao lilijumuisha:
Yezreeli, Kesulothi, Shunemu, 19 Hafaraimu, Shioni, Anaharathi, 20 Rabithi, Kishioni, Ebesi, 21 Remethi, En-Ganimu, En-Hada na Beth-Pasesi.
22 Mpaka ule ukagusa Tabori, Shahasuma na Beth-Shemeshi, na ukaishia kwenye Yordani.
Ilikuwa miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.
23 Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Isakari, kufuatana na koo zao.
Mgawo kwa Asheri
24 Kura ya tano ikaangukia kabila la Asheri, kufuatana na koo zao. 25 Eneo lao lilijumuisha:
Helkathi, Hali, Beteni, Akshafu, 26 Alameleki, Amadi na Mishali. Upande wa magharibi mpaka uligusa Karmeli na Shihor-Libnathi. 27 Tena ukageuka mashariki kuelekea Beth-Dagoni, ukagusa Zabuloni na Bonde la Ifta-Eli, ukaenda upande wa kaskazini hadi Beth-Emeki na Neyeli, ukipitia Kabul upande wa kushoto. 28 Ukaendelea hadi Abdoni, Rehobu, Hamoni na Kana, na kufika Sidoni Kuu. 29 Mpaka huo ukageukia nyuma kuelekea Rama na kwenda hadi kwenye mji wenye ngome wa Tiro, ukageuka kuelekea Hosa na kutokeza baharini katika eneo la Akzibu, 30 Uma, Afeki na Rehobu.
Ilikuwa miji ishirini na mbili, pamoja na vijiji vyake.
31 Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Asheri, kufuatana na koo zao.
Mgawo kwa Naftali
32 Kura ya sita ikaangukia kabila la Naftali, kufuatana na koo zao:
33 Mpaka wao uliendelea kutoka Helefi na kwenye mwaloni ulio Saananimu, ukipitia Adami-Nekebu na Yabineeli hadi Lakumu, na kuishia katika Mto Yordani. 34 Mpaka ukaendelea magharibi kupitia Aznoth-Tabori na kutokea Hukoki. Ukagusa Zabuloni upande wa kusini, Asheri upande wa magharibi, na Yordani upande wa mashariki.
35 Miji yenye ngome ilikuwa Sidimu, Seri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi, 36 Adama, Rama, Hazori, 37 Kedeshi, Edrei, na En-Hasori, 38 Ironi, Migdal-Eli, Horemu, Beth-Anathi na Beth-Shemeshi.
Kulikuwa na miji kumi na tisa na vijiji vyake.
39 Miji hiyo pamoja na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Naftali, kufuatana na koo zao.
Mgawo kwa Dani
40 Kura ya saba ikaangukia kabila la Dani, kufuatana na koo zao. 41 Eneo la urithi wao lilijumuisha:
Sora, Eshtaoli, Iri-Shemeshi, 42 Shaalabini, Aiyaloni, Ithla, 43 Eloni, Timna, Ekroni, 44 Elteke, Gibethoni, Baalathi, 45 Yehudi, Bene-Beraki, Gath-Rimoni, 46 Me-Yarkoni na Rakoni, pamoja na eneo linalotazamana na Yafa.
47 (Lakini Wadani walipata shida kulimiliki eneo lao; kwa hiyo walipanda kuishambulia Leshemu, wakaitwaa, wakawaua watu wake kwa upanga na kuukalia. Walikaa Leshemu na kuuita Dani kufuatana na jina la baba yao.)
48 Miji hii na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Dani, kufuatana na koo zao.
Mgawo kwa Yoshua
49 Walipomaliza kuigawa nchi kulingana na sehemu zilizowaangukia, Waisraeli walimpa Yoshua mwana wa Nuni urithi kati yao, 50 kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa ameamuru. Walimpa mji alioutaka, ambao ni Timnath-Sera*Unajulikana pia kama Timnath-Heresi(taz. Yoshua 24:30; Waamuzi 2:9). ulio katika nchi ya vilima ya Efraimu. Naye akajenga mji, akakaa huko.
 
51 Haya ndio maeneo ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa koo za makabila ya Israeli waliyagawanya kwa kura huko Shilo mbele za Mwenyezi Mungu, penye ingilio la Hema la Kukutania. Hivyo wakamaliza kuigawanya nchi.

*19:50 Unajulikana pia kama Timnath-Heresi(taz. Yoshua 24:30; Waamuzi 2:9).