Zaburi 117
Sifa za Mwenyezi Mungu
1 Msifuni Mwenyezi Mungu, enyi mataifa yote;
mtukuzeni yeye, enyi watu wote.
2 Kwa kuwa upendo wake kwetu ni mkuu,
uaminifu wa Mwenyezi Mungu unadumu milele.
Msifuni Mwenyezi Mungu.*kwa Kiebrania ni Hallelu Yah.