Zaburi 131
Kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.
1 Moyo wangu hauna kiburi, Ee Mwenyezi Mungu,
macho yangu hayajivuni;
sijishughulishi na mambo makuu kunizidi
wala mambo ya ajabu mno kwangu.
2 Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu;
kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake,
kama mtoto aliyeachishwa kunyonya
ndivyo ilivyo nafsi iliyo ndani yangu.
3 Ee Israeli, mtumaini Mwenyezi Mungu
tangu sasa na hata milele.