8
Laiti ungekuwa kwangu kama ndugu wa kiume,
ambaye aliyanyonya matiti ya mama yangu!
Kisha, kama ningekukuta huko nje,
ningekubusu,
wala hakuna mtu yeyote angenidharau.
Ningekuongoza na kukuleta
katika nyumba ya mama yangu,
yeye ambaye amenifundisha.
Ningekupa divai iliyokolezwa unywe,
asali ya maua ya mikomamanga yangu.
Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu,
na mkono wake wa kuume unanikumbatia.
Binti za Yerusalemu, ninawaagiza:
msichochee wala kuamsha mapenzi
hata yatakapotaka yenyewe.
 
Rafiki
Ni nani huyu anayekuja kutoka nyikani
akimwegemea mpenzi wake?
Mpendwa
Nilikuamsha chini ya mtofaa,
huko mama yako alipotunga mimba yako,
huko yeye alipata uchungu akakuzaa.
Nitie kama muhuri moyoni mwako,
kama muhuri kwenye mkono wako;
kwa maana upendo una nguvu kama mauti,
wivu wake ni mkatili kama Kuzimu*Kuzimu kwa Kiebrania ni Sheol, yaani Shimo lisilo na mwisho..
Unachoma kama mwali wa moto,
kama mwali mkubwa wa moto wa Mwenyezi Mungu hasa.
Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo,
mito haiwezi kuugharikisha.
Kama mtu angetoa mali yote ya nyumbani mwake
kwa ajili ya upendo,
angedharauliwa kabisa.
Rafiki
Tunaye dada mdogo,
matiti yake hayajakua bado.
Tutafanya nini kwa ajili ya dada yetu
wakati atakapokuja kuposwa?
Kama yeye ni ukuta,
tutajenga minara ya fedha juu yake.
Na kama yeye ni mlango,
tutamzungushia mbao za mwerezi.
Mpendwa
10 Mimi ni ukuta,
nayo matiti yangu ni kama minara.
Ndivyo ambavyo nimekuwa machoni pake
kama yule anayeleta utoshelevu.
11 Sulemani alikuwa na shamba la mizabibu huko Baal-Hamoni;
alikodisha shamba lake la mizabibu kwa wapangaji.
Kila mmoja angeleta kwa ajili ya matunda yake
shekeli elfu mojaShekeli 1,000 ni kama kilo 11.5. za fedha.
12 Lakini shamba langu la mizabibu
ambalo ni langu mwenyewe
ni langu kutoa;
hizo shekeli elfu moja ni kwa ajili yako, ee Sulemani,
na shekeli mia mbiliShekeli 200 ni kama kilo 2.3. ni kwa ajili
ya wale wanaotunza matunda yake.
Mpenzi
13 Wewe ukaaye bustanini
pamoja na rafiki mliohudhuria,
hebu nisikie sauti yako!
Mpendwa
14 Njoo, mpenzi wangu,
uwe kama paa
au kama ayala mchanga
juu ya milima iliyojaa manukato.

*8:6 Kuzimu kwa Kiebrania ni Sheol, yaani Shimo lisilo na mwisho.

8:11 Shekeli 1,000 ni kama kilo 11.5.

8:12 Shekeli 200 ni kama kilo 2.3.