9
1 Yesu akaingia kwenye boti, akavuka na akafika kwenye mji alipokuwa anaishi.
2 Tazama, wakamletea mtu aliyepooza amelazwa kwenye godoro. alipooiona imani yao, Yesu akamwambia mtu aliyepooza, “Mwanangu, uwe na furaha, Dhambi zako zimesamehewa”
3 Tazama, Baadhi ya walimu wa sheria wakasemezana wao kwa wao, “Huyu mtu anakufuru”
4 Yesu akatambua mawazo yao na kusema, “Kwa nini mnawaza maovu moyoni mwenu?
5 Kipi kilicho rahisi kusema, 'Dhambi zako zimesamehewa' au kusema, 'Simama na utembee?'
6 Lakini mtambue ya kwamba Mwana wa Adamu anao uwezo wa kusamehe dhambi...” aliyasema haya kwa yule aliyepooza, “Simama, chukua godoro lako, na uende nyumbani kwako”
7 Ndipo yule mtu akasimama na kuondoka kwenda nyumbani kwake.
8 Makutano walipoona hayo, walishangaa na kumsifu Mungu, ambaye amewapa uwezo huo watu.
9 Na Yesu alipokuwa akipita kutoka hapo, alimwona mtu ambaye aliitwa kwa jina la Mathayo, ambaye alikuwa amekaa sehemu ya watoza ushuru. Naye akamwambia, “Nifuate mimi” Naye akasimama na kumfuata.
10 Na Yesu alipoketi ili ale chakula ndani ya nyumba, wakaja watoza ushuru wengi na watu waovu wakashiriki chakula pamoja na Yesu na wanafunzi wake.
11 Ndipo Mafarisayo walipoona hayo, wakawaambia wanafunzi “Kwa nini mwalimu wenu anakula chakula pamoja na watoza ushuru na watu waovu?”
12 Yesu aliposikia hayo, naye alisema “ Watu walio na afya nzuri hawahitaji mganga, isipokuwa wale walio wagonjwa.
13 Inawapasa muende mkajifunze maana yake, “Ninapenda rehema na siyo dhabihu” Kwa kuwa nilikuja, si kwa wenye haki kutubu, lakini kwa wenye dhambi.
14 Ndipo wanafunzi wa Yohana wakaja kwake na kusema, “Kwa nini sisi na mafarisayo tunafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?”
15 Yesu akawaambia, Je wasindikizaji wa arusi wanaweza kuwa na huzuni pindi Bwana arusi anapokuwa pamoja nao? Lakini siku zinakuja ambapo Bwana arusi atachukuliwa kutoka kwao, na ndipo watakapofunga.
16 Hakuna mtu anayeweka kipande cha nguo mpya kwenye nguo ya zamani, kiraka kitatatuliwa kutoka kwenye nguo na mpasuko mkubwa utatokea.
17 Hakuna watu wanaoweka mvinyo mpya katika chombo cha mvinyo wa zamani, ikiwa watafanya, ngozi itachanika, mvinyo utatoweka na ngozi itaharibika. Badala yake, huweka mvinyo mpya katika ngozi mpya na vyote vitakuwa salama.
18 Wakati Yesu alipokuwa akiwaambia mambo hayo, tazama, afisa akaja akasujudu mbele yake, Naye akasema, “ Binti yangu amefariki punde, lakini njoo na uweke mkono wako juu yake na yeye ataishi tena.
19 Ndipo Yesu akasimama na kumfuata na wanafunzi wake pia.
20 Tazama, mwanamke ambaye alikuwa anatokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja karibu na Yesu na akagusa sehemu ya pindo la vazi lake.
21 Kwa kuwa alisema, “Endapo nitagusa vazi lake, nami nitapata uponyaji.”
22 Yesu akageuka na kumtazama na kumwambia. “Binti, jipe moyo, imani yako imekufanya upone,” Na muda huo huo mwanamke akapata uponyaji muda huo.
23 Na Yesu alipofika kwenye nyumba ya afisa, naye aliwaona wapiga tarumbeta na umati wa watu ulikuwa ukipiga kelele.
24 Naye akasema, “Tokeni hapa, kwa kuwa binti hajafa, bali amelala. Lakini wao walicheka na kumkebehi.
25 Na wale watu walipotolewa nje, naye akaingia chumbani na kumshika mkono na msichana akaamka.
26 Na habari hizi zikaenea katika mji mzima.
27 Ndipo Yesu alipokuwa akipita kutoka pale, wanaume wawili vipofu wakamfuata. Waliendelea kupaza sauti wakisema, “Tunaomba uturehemu, Mwana wa Daudi.”
28 Pindi Yesu apokuwa amefika kwenye nyumba, wale vipofu wakaja kwake. Yesu akawaambia, “Mnaamini kwamba ninaweza kutenda?” Nao wakamwambia “Ndiyo, Bwana”
29 Ndipo Yesu akagusa macho yao na kusema “Na ifanyike hivyo kwenu kama imani yenu ilivyo”
30 Na macho yao yakafumbuka. Ndipo Yesu akasisitiza akawaamuru na kusema “Angalieni mtu yeyote asifahamu kuhusu jambo hili.”
31 Lakini watu hawa wawili wakaondoka na kutangaza habari hizi sehemu zote za mji.
32 Ndipo wale wanaume wawili walipokuwa wakienda zao, Tazama, mtu mmoja bubu aliyepagawa na pepo akaletwa kwa Yesu.
33 Na pepo walipomtoka, yule mtu bubu akaanza kuongea. Umati ukashangazwa na kusema “Hii haijawahi kutokea katika Israel.
34 Lakini mafarisayo walikuwa wakisema “ Kwa wakuu wa pepo, anawafukuza mapepo”
35 Yesu akaenda kwenye miji yote na vijiji. Naye akaendelea kufundisha katika masinagogi, akihubiri injili ya ufalme, na kuponya magonjwa ya kila aina na udhaifu wa aina zote.
36 Wakati alipotazama umati, naye aliwaonea huruma, kwa sababu walisumbuka na kuvunjika moyo. Walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji.
37 Naye akawaambia wanafunzi wake. “Mavuno ni mengi, lakini wafanya kazi ni wachache.
38 Hivyo basi upesi mwombeni Bwana wa mavuno, ili kwamba atume wafanya kazi katika mavuno yake.”