28
Zaburi ya Daudi. Kwako,
1 Yahwe, ninalia; mwamba wangu, usinipuuze. Ikiwa haunijibu, nitaungana na wale waendao chini kaburini.
2 Sikia kilio cha kusihi kwangu pale niitapo msaada kutoka kwako, niinuapo mikono yangu mbele ya mahali patakatifu zaidi!
3 Usiniburute pamoja na waovu, wale wafanyao uovu, waongeao amani na majirani zao lakini mioyoni mwao mna uovu.
4 Uwape kulingana na sitahili ya matendo yao na uwalipe kulingana na madai ya maovu yao, uwalipe kwa ajili ya kazi ya mikono yao na uwape kile wanachostahili.
5 Kwa sababu hawayaelewi matendo ya Yahwe wala kazi ya mikono yake, atawakanyaga kanyaga chini na hata wajenga tena wao.
6 Abarikiwe Yahwe kwa sababu yeye amesikia sauti ya kusihi kwangu!
7 Yahwe ni nguvu yangu na ngao yangu; moyo wangu wa humwamini yeye, na ninasaidiwa. Kwa hiyo moyo wangu hufurahia sana, nami nitamsifu yeye kwa kuimba.
8 Yahwe ni nguvu ya watu wake, naye ni mkombozi salama wa wapakwa mafuta wake.
9 Uwaokoe watu wako na uwabariki warithi wako. Uwe mchungaji wao na uwabebe milele.