41
Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi.
1 Amebarikiwa mtu yule amkumbukaye mnyonge; katika siku ya taabu, Yahwe atamuokoa.
2 Yahwe atamuhifadhi na kumuweka hai, naye atabarikiwa duniani; Yahwe hata mrudisha kwenye mapenzi ya adui zake.
3 Awapo kwenye kitanda cha mateso Yahwe atamsaidia; nawe utakifanya kitanda cha ugonjwa kuwa kitanda cha uponyaji.
4 Nami nilisema, “Yahwe unihurumie! Uniponye, kwa maana nimekutenda dhambi wewe.”
5 Adui zangu huongea maovu dhidi yangu, wakisema, 'Atakufa lini na jina lake lipotee?'
6 Adui yangu ajapo kuniona, huongea mambo yasiyo na maana; moyo wake hukusanya maafa yangu kwa ajili yake mwenyewe; na aondokapo kwangu, yeye huwaambia watu wengine kuhusu hayo.
7 Wale wote wanaonichukia kwa pamoja hunon'gona dhidi yangu; nao wanafarijika kwa ajili ya maumivu yangu.
8 Wakisema, “Gonjwa baya limemshikilia yeye haswa; na sasa kuwa amelala kitandani, hatainuka kamwe.”
9 Kweli, hata rafiki yangu wa karibu, ambae nilimuamini, aliye kula mkate wangu, ameinua kisigino chake dhidi yangu.
10 Bali wewe, Yahwe, unihurumie na uniinue ili kwamba niwalipizie kisasi.
11 Na hivi nitajua kuwa unafurahishwa nami, kwa kuwa adui yangu hatafurahia kunishinda.
12 Kwangu mimi, wewe unanisaidia katika uadilifu wangu na utaniweka mbele ya uso wako milele.
13 Yahwe, Mungu wa Israeli asifiwe milele na milele. Amen na Amen. Kitabu ya Pili