87
Zaburi ya wana wa Kora; wimbo.
1 Mji aliouanzisha umesimama juu ya mlima mtakatifu;
2 Yahwe anapenda zaidi malango ya Sayuni kuliko mahema yote ya Yakobo.
3 Mambo matukufu yamesemwa kwako, mji wa Mungu. Selah
4 Ninataja Rahabu na Babeli kwa wafuasi wangu. Tazama, Filisti, na Tiro, pamoja na Ethiopia nao watasema, 'Huyu alizaliwa humo.'”
5 Itasemwa juu ya Sayuni, “Kila mmoja wa hawa alizaliwa katika yeye; na yeye Aliye Juu atamuimarisha.
6 Yahwe anaandika katika kitabau cha sensa ya mataifa, “Huyu alizaliwa humo.” Selah
7 Hivyo waimbaji na wachezaji kwa pamoja waseme, “chemchem zangu zimo kwako.”