6
Israeli asiye tubu 
  1 “Njooni, tumrudie Mwenyezi Mungu.  
Ameturarua vipande vipande  
lakini atatuponya;  
ametujeruhi lakini  
atatufunga majeraha yetu.   
 2 Baada ya siku mbili atatufufua;  
katika siku ya tatu atatuinua,  
ili tuweze kuishi mbele zake.   
 3 Tumkubali Mwenyezi Mungu,  
tukaze kumkubali yeye.  
Kutokea kwake ni hakika kama vile  
kuchomoza kwa jua;  
atatujia kama mvua za masika,  
kama vile mvua za vuli  
ziinyweshavyo nchi.”   
 4 “Nifanye nini nawe, Efraimu?  
Nifanye nini nawe, Yuda?  
Upendo wako ni kama ukungu wa asubuhi,  
kama umande wa alfajiri utowekao.   
 5 Kwa hiyo nimewakata ninyi vipande vipande  
nikitumia manabii wangu;  
nimewaua ninyi kwa maneno ya kinywa changu,  
hukumu zangu zinawaka  
kama umeme juu yenu.   
 6 Kwa maana nataka rehema, wala si dhabihu,  
na kumkubali Mungu  
kuliko sadaka za kuteketezwa.   
 7 Wamevunja agano kama Adamu:  
hawakuwa waaminifu kwangu huko.   
 8 Gileadi ni mji wa watenda maovu,  
umetiwa madoa kwa nyayo za damu.   
 9 Kama wanyang’anyi wamviziavyo mtu,  
ndivyo magenge ya makuhani wafanyavyo;  
wanaulia watu kwenye njia iendayo Shekemu,  
wakifanya uhalifu wa aibu.   
 10 Nimeona jambo la kutisha  
katika nyumba ya Israeli.  
Huko Efraimu amejitolea kwa ukahaba  
na Israeli amenajisika.   
 11 “Pia kwa ajili yako, Yuda,  
mavuno yameamriwa.  
“Wakati wowote ningerejesha neema ya watu wangu,