12
Orodha ya wafalme walioshindwa
1 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kumiliki maeneo yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni hadi Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki mwa Araba:
2 Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.
Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi.
3 Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi*yaani Bahari ya Galilaya hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi†yaani Bahari Mfu), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya miteremko ya Pisga.
4 Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.
5 Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa Wageshuri, na Wamaaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.
6 Musa, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.
7 Hawa ndio wafalme ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao. 8 Nchi hizi ni: nchi ya vilima, Shefela‡au upande wa magharibi chini ya vilima, Araba, miteremko ya milima, jangwa, na Negebu; yaani nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi.
Wafalme hawa walikuwa:
9 mfalme wa Yeriko;
mfalme wa Ai (karibu na Betheli);
10 mfalme wa Yerusalemu;
mfalme wa Hebroni;
11 mfalme wa Yarmuthi;
mfalme wa Lakishi;
12 mfalme wa Egloni;
mfalme wa Gezeri;
13 mfalme wa Debiri;
mfalme wa Gederi;
14 mfalme wa Horma;
mfalme wa Aradi;
15 mfalme wa Libna;
mfalme wa Adulamu;
16 mfalme wa Makeda;
mfalme wa Betheli;
17 mfalme wa Tapua;
mfalme wa Heferi;
18 mfalme wa Afeki;
mfalme wa Lasharoni;
19 mfalme wa Madoni;
mfalme wa Hazori;
20 mfalme wa Shimron-Meroni;
mfalme wa Akshafu;
21 mfalme wa Taanaki;
mfalme wa Megido;
22 mfalme wa Kedeshi;
mfalme wa Yokneamu katika Karmeli;
23 mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori);
mfalme wa Goimu katika Gilgali;
24 mfalme wa Tirsa;
jumla ya wafalme thelathini na mmoja (31).