Zaburi 95
Wimbo wa kumsifu Mwenyezi Mungu
Njooni, tumwimbie Mwenyezi Mungu kwa furaha;
tumfanyie kelele za shangwe
Mwamba wa wokovu wetu.
Tuje mbele zake kwa shukrani,
tumtukuze kwa vinanda na nyimbo.
 
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni Mungu mkuu,
mfalme mkuu juu ya miungu yote.
Mkononi mwake mna vilindi vya dunia,
na vilele vya milima ni mali yake.
Bahari ni yake, kwani ndiye aliyeifanya,
na mikono yake iliumba nchi kavu.
 
Njooni, tusujudu, tumwabudu,
tupige magoti mbele za Mwenyezi Mungu Muumba wetu,
kwa maana yeye ndiye Mungu wetu,
na sisi ni watu wa malisho yake,
kondoo chini ya utunzaji wake.
 
Mkiisikia sauti yake leo,
msiifanye mioyo yenu migumu
kama mlivyofanya kule Meriba*maana yake Kugombana,
kama mlivyofanya siku ile
kule Masamaana yake Kujaribiwa jangwani,
ambapo baba zenu walinijaribu na kunipima,
ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu.
10 Kwa miaka arobaini nilikasirikia kizazi kile,
nikasema, “Hawa ni taifa ambalo mioyo yao imepotoka,
nao hawajazijua njia zangu.”
11 Hivyo nikatangaza kwa kiapo katika hasira yangu,
“Kamwe hawataingia rahani mwangu.”

*Zaburi 95:8 maana yake Kugombana

Zaburi 95:8 maana yake Kujaribiwa