Zaburi 134
Wito wa kumsifu Mwenyezi Mungu
Wimbo wa kwenda juu.
Msifuni Mwenyezi Mungu, ninyi nyote watumishi wa Mwenyezi Mungu,
ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu.
Inueni mikono yenu katika patakatifu
na kumsifu Mwenyezi Mungu.
 
Naye Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na dunia,
awabariki kutoka Sayuni.